Mchezaji Miquissone Apelekwe tu KMC Kwa Mkopo - Mchambuzi
Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia runinga ya TV3, Boiboi Mkali, ameushauri uongozi wa Klabu ya Simba kuwa wamtoe mchezaji wao, Luis Jose Miquissone kwa mkopo kwenda Klabu ya KMC.
Boiboi amesema hayo mara baada ya kushuhudia kiwango cha Luis wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC hivi karibuni dhidi ya Coastal Union ambapo mchezaji huyo raia wa Msumbiji alitoa pasi ya bao na kusababisha penati iliyozaa bao na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 3-0.
"Nilitumia mchezo kati ya Simba dhidi ya Coastal Union kumwangilia kwa umakini kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Miquissone katika mchezo huo, Bado ni mchezaji ambaye anaonekana kwa uchezaji wake bado hajaimalika kama alivyokuwa awali.
"Uongozi wa Simba inabidi wachukue hatua kwa Miquissone kwaajili ya kumrudisha katika kuwango chake, Ndani ya kikosi cha Simba bado hana nafasi ya kucheza mara kwa mara kutokana na ubora na viwango vya wachezaji wengine katika eneo la ushambuliaji.
"Miquissone anatakiwa atolewe kwa mkopo katika klabu ya Kmc iliapate nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza na kupata dakika za kutosha ili kurudisha kiwango chake.
"Katika klabu ya KMC kuna kocha mkuu wa klabu hiyo ABDI HAMID MOALLIN ni kocha ambaye yuko vizuri kuboresha viwango vya wachezaji na kumpa mbinu nyingi zenye ubora kiufundi, Nafikli itamjenga Miquissone katika kipindi atakapo kuwepo klabuni KMC," amesema Boiboi Mkali.