Mke Adai Huwa Anamnyonyesha Mume Wake Maziwa yake, Kumeimarisha ndoa




Rachel Bailey(30) kutoka Florida, Marekani ambaye ni mama wa watoto watatu anasema mwaka 2016 akiwa ananyonyesha mtoto wake wa kwanza yeye na mume wake kwa jina la Alexernda(30) walisafiri peke yao, na akiwa safarini sababu alimuacha mtoto nyumbani, maziwa yalijaa hakuwa amebeba kifaa maalum cha kuyatoa(pampu),ilifikia muda akawa anaumia sana na kuingiwa na wasiwasi anaweza kupata maradhi

Kama utani wakakubaliana na mume wake huyo ayanyonye maziwa kumsaidia na akafanya hivyo akapata ahueni vizuri, kuanzia hapo ikawa ndio zao wanandoa hao kila maziwa yakimjaa Rachel mume anayanyonya 😳

Hata walipopata watoto wengine wawili miaka ya baadaye bado mume alikuwa ananyonyeshwa ila huwa ni baada ya watoto kunyonya wakaridhika

Mume huyo anasema maziwa ya mke wake yapo tofauti na maziwa ya ngombe ila amesbayazoea na anayapenda

Rachel anasema haoni ni kitu cha ajabu kwao maana mume wake hajawahi kuumwa, sana sana watu wanamsifia mumewe kazidi kuwa na muonekano mzuri ikiwemo ngozi nene yenye afya kama yote akieleza kuwa maziwa yake yamejaa virutubisho

Rachel anasema kumnyonyesha mume wake kumezidi kuimarisha ndoa yao kwani kumezidi kuwapa ukaribu, tangu mtoto wa kwanza hadi wa tatu mume wake kwa siku alikuwa ananyonya maziwa kwa siku mara tatu hadi mara nne baada ya watoto kunyonya kwani Rachel huwa anatoa maziwa mengi anapokuwa amejifungua

Lakini kwasasa maziwa yamepungua mume wake ananyonya mara moja tu kwa siku muda wa usiku hasa wakiwa kitandani

Amesisitiza hawatafuti kiki wala umaarufu ila huo ndio ukweli kumyonyesha mume kwa kwa lengo la kumsaidia kupunguza maziwa na maumivu katika mazingira yaliyokuwa nje ya uwezo wake kumepelekea kuzidi kuimarika kwa ndoa yao

Watoto wao kuna wa miaka 7, 6 na 2

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad