Mkubwa Fella Afunguka Wasafi Kutokwenda Kumzika Haitham


Mkubwa Fella Afunguka Wasafi Kutokwenda Kumzika Haitham

Meneja wa Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz aitwaye Mubwa Fella amekiri kuwa Wasafi hawakwenda kwenye mazishi ya msanii mwenzao, Haitham Ghazal Seif 'Haitham Kim' ambaye alifariki hivi karibuni na kuzikwa kwatika makaburi ya Kisutu.


Mkubwa Fella amejibu hayo wakati akihojiwa na vyombo vya habari mkoani Ruangwa ambapo Timu nzima ya Wasafi ilikwenda kwa ajili ya Tamasha la Wasafi Festival huku akiongeza kuwa wamepanga kufanya kitu kikubwa kwa familia ya marehemu Haitham.


"Ni kweli hatukuhudhulia mazishi ya Haitham Kim lakini hiyo haimaanishi hatujashiriki, kushiriki msiba siyo tu kwenda makaburini kuzika wala kwenda kukaa nyumbani kwa Marehemu.


"Sisi kama Wasafi hatukuonekana msibani lakini tuna mpango wa kuifanyia kitu familia ya marehemu Haitham Kim," amesema Mkubwa Fella.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad