Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umeunda Kamati Maalum kwa ajili ya Maandalizi ya Uchaguzi wa Chipukizi wa CCM Taifa unaotarajiwa kufanyika December 2023 ambapo umempitisha Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo huku Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Hassan Bomboko akipitishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida ameongoza kikao kilichopitisha uamuzi huo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam ambapo pia amezindua Kamati za Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi 2023/2027.
Kamati zilizoundwa, kuzinduliwa na kupewa baraka za Jumuiya kuanza Majukumu kwa Ustawi wa Uchumi wa Jumuiya ni Kamati ya Uwezeshaji Uchumi na Fedha, ambayo itaongozwa na Maria Sebastian na Makamu Mwenyekiti wake Ayoub Mohamed Mahamood pamoja na Wajumbe wengine ambao wameteuliwa kuwepo kwenye Kamati hiyo.
Kamati nyingine ni ya Uhakiki wa Mali za Jumuiya Umoja wa Vijana wa Chama ambayo itaongozwa na Mwenyekiti Zuwena Amour Suleiman, na Makamu Mwenyekiti, Adestino Mwilinge pamoja na Wajumbe wengine ambao wameteuliwa kuwepo kwenye Kamati hiyo