MPYA: Watanzania waliofariki ajali ya moto Afrika Kusini wafikia sita

MPYA: Watanzania waliofariki ajali ya moto Afrika Kusini wafikia sita


Idadi ya Watanzania waliofariki katika ajali ya moto iliyotokea Alhamisi wiki iliyopita nchini Afrika Kusini, imeongezeka hadi kufikia 6 huku zoezi la kutambua miili likiendelea.


Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam, Balozi wa Tanzania nchini humo, Meja Jenerali mstaafu, Gaudence Milanzi, amesema idadi ya vifo imeongezeka kutoka 74 hadi 77.


“Suala la utambuzi linaendelea na limetokana na ushirikiano kati ya ubalozi na maafisa wa Serikali ya Afrika Kusini, mpaka sasa tumetambua miili sita za Watanzania,” amesema Milanzi.


Kuhusu taratibu za kusafirisha miili ya Watanzania hao kwa ajili ya maziko nchini, Balozi Milanzi amesema kuwa bado hawajaanza taratibu hizo, isipokuwa wameanza kufanya taratibu za kujua ndugu wa waliofariki.


“Hatuwezi kusafirisha kabla hatujajua ndugu zao ni kina na nani, tukikamilisha hilo ndipo tutatangaza utaratibu mzima wa kusafirisha,” amesema balozi huyo.


Aidha amesema majeruhi Watanzania wanaendelea vizuri kufuatia huduma ambazo wamekuwa wakipatiwa na Serikali nchini humo.


Pia amesema Serikali hiyo imewapatia hifadhi waliokuwa wakiishi katika jengo ambalo liliungua moto huku baadhi ya waathiriwa wakikataa kuhifadhiwa kwa kuhofia kukaguliwa uraia wao.


“Wengine hawakupenda kuhifadhiwa, hatujui hata wako wapi. Wana hofu ya kumatwa kwa kutokuwa na vibali. Waliokubali wanaendelea kupata huduma za afya na vyakula,” ameongeza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad