Msemaji Ahmed Ally Afunguka Kuhusu Kauli ya Mashabiki wa SIMBA Kudai Wanashinda ila Hawana Furaha

  

Msemaji Ahmed Ally Afunguka Kuhusu Kauli ya Mashabiki wa SIMBA Kudai Wanashinda ila Hawana Furaha

Mpira wa miguu kilele chake huwa ni ushindi (kupata alama tatu au kwenye mashindano ni kufuzu hatua inayofuata), kwenye Ligi tumechukua alama tatu dhidi ya Mtibwa Sugar, Dodoma Jiji na Coastal Union.

Kwa hiyo ukija kwenye malengo, bado tupo kwenye malengo ambayo ni kushinda mechi kadiri tuwezavyo. Watu wanataka timu ifunge magoli mengi, msimu uliopita tulifunga magoli mengi na hatukuwa mabingwa.

Huyu ambaye anasema tunashinda lakini hatuna furaha, itakuaje kama tutaendelea kushinda na kuwa mabingwa, atakuja kusema hana furaha ya ubingwa? Acha tuendelee kuishi kwenye malengo makuu ambayo ni kushinda kila mechi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad