Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya amemtaka Mwalimu Japhet Maganga kurejea kazini kufuatia Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Juma Mkomi kutoidhinisha maombi ya mwalimu huyo kupata kibali cha kuazimwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mabelya, Maganga ni muajiriwa wa Manispaa ya Temeke katika nafasi ya ualimu na aliomba kibali cha kuazimwa kwa vipindi tofauti vya miaka mitatu, kuanzia mwaka 2017- 2020, kisha 2020 hadi Septemba 30, 2023.
“Mwalimu Maganga aliomba tena kibali cha kuazimwa kwa mara ya tatu ambapo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi hajaridhia maombi hayo,
“hivyo, Mwalimu Maganga M. Japhet anapaswa kurejea kwenye kituo chake cha kazi mara moja, mnamo tarehe 01, Oktoba 2023,” kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Manispaa ya Temeke.
Itakumbukwa mnamo Januari 25, 2023, Maganga aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, ingali ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) lakini hakuafikiana na uteuzi huo