"Assalam Aleykum ndugu zangu na Watanzania wote, tumepokea taarifa ya msiba kutoka kwa msanii mwenzetu Haitham Kim ambaye amefariki dunia mchana wa leo poleni sana. Lakini kifo ni mawaidha, kifo ni ukumbusho kuwa wakati wowote tunaondoka duniani tumejiandaaje?"
"Nataka niongee na wasanii, Wasanii hamna umoja na hamjajipanga kwenye kesho yenu, niwakumbushe tu Haitham alipitia changamoto ya maradhi ya kuumwa lakini baadae akawa hayuko vizuri kiuchumi akahitaji msaada. Nilichukizwa sana kuona Wasanii wanamposti msanii mwenzao mgonjwa eti wanaomba msaada wanaweka na namba. Nilichukizwa sana, ni kitendo ambacho siyo kizuri kabisa cha kuanika matatizo ya mtu ulimwenguni"
"Wasanii mlipaswa muunde kikundi muitane kama vile mnavyoitana kwenye kumbi za starehe kila msanii angetoa shilingi milioni moja ambapo kwa wasanii 30 tungepata milioni 30 ambazo zingeweza kutibu matibabu yake au mgefanya show moja mapato mngemsaidia mwenzenu apone kuliko kumuanika mwenzenu mnawambia Watanzania wamchangie🙄 nyie mlichanga?
hii ni mbaya na ni lazima mkubali hilo kwamba hamna umoja, mjifunze kupitia hili na muwe na mahusiano mazuri na jamii"- Mwijaku