Nape amshukuru Rais Samia kwa 'kutoboa' kwenye mkeka wa mawaziri

  
Nape amshukuru Rais Samia kwa 'kutoboa' kwenye mkeka wa mawaziri

Nape amshukuru Rais Samia kwa 'kutoboa' kwenye mkeka wa mawaziri

Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumbakiza kwenye Baraza la Mawaziri hata baada ya mabadiliko madogo ya Baraza hilo aliyoyafanya hivi karibuni.


Nape ametoa shukrani hizo mbele mbele ya Rais Samia wakati wa uzinduzi wa Jengo la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) leo September 02,2023, Jijini Arusha.


“Mh. Rais karibu Arusha, nilikuja Arusha Aug 30,2023 wakati natoka Dodoma nikiwa njiani Katibu Mkuu akanitumia mkeka, nilipouona mkeka nikamwambia Dereva simama kidogo, nikaongeza AC ya gari nikaanza kusomaa mpaka mwisho nikaona nimetoboa, nikaangalia Naibu wangu nae katoboa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu nao wametoboa, Mh. Rais nimesimama kwa unyenyekevu mkubwa kukushukuru kwa kutuamini Mimi na wenzangu”


“Asante kwa kutupa heshima na imani na dhamana ya kuendelea kuongoza Sekta hizi nakuhakikishia kwa niaba ya wenzangu tutatimiza ndoto zako na za Watanzania na hatutokuangusha Mh. Rais”


“Nakushukuru kwa kukubali kuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jengo la Umoja wa Posta Afrika”


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad