Paul Pogba Asimamishwa Kucheza Soka, Kisa Matumizi ya Dawa za Kuongeza Nguvu


Kiungo wa Juventus, Mfaransa Paul Pogba, amesimamishwa kwa muda kucheza Soka, kutokana na kukutwa na hatia ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu ambazo zimezuiliwa michezoni.

Kipimo, kilichofanywa baada ya ushindi wa Juve dhidi ya Udinese, mechi iliochezwa mwezi Agosti mwaka huu, kilitambua uwepo wa Testosterone, Homoni ambayo huongeza nguvu (endurance), kinyume na Sheria, kwa Pogba ambaye alianzia benchi katika mchezo huo.

Taasisi ya kupambana na Dawa za kuongeza nguvu michezoni nchini Italia, leo imefikia uamuzi huo dhidi ya Pogba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad