Pili: Kama Mwanaume Wako Hakuchiti Achana nae Hakufai

 

Pili: Kama Mwanaume Wako Hakuchiti Achana nae Hakufai

Msanii maarufu wa maigizo nchini, matata wa kike Bongo, Gladness Joasy Kifaluka ‘Pili Kitimtim’ ametoa ujumbe kuwa iwapo mwanamke yupo kwenye mahusiano na mpenzi wake hamcheat, basi aachane naye.


Pili ambaye pia ni mjasiriamali na producer anayemiliki Tuzo ya Mchekeshaji Bora wa wa Kike wa mwaka 2022/23, Series bora ya vichekesho 2021/23 na mwanzilishi wa Kitimtim Shoo amesema ukiwa kwenye mahusiano lazima mwenza wako atatafutwa tu na wanaume wengine, kwa hivyo ukiona hivyo unapaswa kujisifia kuwa una mwanaume anayependwa na kuwavutia wanawake wengine.


"Kama mwanamke una mahusiano yaliyopoa achana nayo, bwana ambaye ukishika simu yake hukutani na meseji za wanawake wanaomtongoza achana nae huyo umesusiwa, wanawake wamekususia.


"Unatakiwa kuwa na mwanaume ambaye ana mahusiano pembeni ukishika simu yake ukutane na meseji mchanganyiko mara I miss you, baby nimeshafika gest, huyo mkeo anayekoroma mpaka nyumba inatoka vismenti ameshalala tuondoke!!!"


"Unapata hasira damu inachemka mapigo ya moyo yanapiga, huyu ndo mwanaume unayetakuwa kuwa nae kwenye mahusiano ili uchangamke usizeeke mapema"- Pili Kitimtim.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad