Polisi Waanza Uchunguzi Aliyejirusha Ghorofa ya saba

 


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema jeshi hilo linaendelea kuchunguza tukio la Chadi Nsanda, aliyenusurika kifo baada ya kudaiwa kujirusha kutoka ghorofa ya saba katika jengo la Shirika la Bima (NIC), jijini Dar es Salaam.


Tukio la kujirusha Chadi ambaye ni dereva wa mmoja wa bosi wa taasisi hiyo, lilitokea Jana, Septemba 05, mwaka huu, baada ya majibizano ya muda mrefu na bosi huyo, baada ya kuuliza ilipo kompyuta ya bosi huyo inayodaiwa kupotea.


Akizungumza na Mwananchi, Kamanda Muliro ameeleza tukio hilo lilitokea jioni na Chadi alijirusha kupitia dirishani na kudondokea kwenye paa la jengo la mgahawa, lilipo jirani na jengo hilo.


“Hakuangukia kwenye simenti na bado yupo hai, na amelazwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi).Tunaendelea kuchunguza na baada ya kumaliza kupata matibabu yake tutamuhoji kwa kina,” amesema.


Kamanda ameeleza kuwa taarifa za awali zinadai sababu ya dereva huyo kujirusha kulikuwa na mahojiano na mwajiri wake kufuatia kupotea kompyuta mpakato na kwamba Chadi alikuwa mtuhumiwa.


“Pale chini kuna ulinzi na alipotoka siku moja kabla ya tukio ndani ya jengo hilo, alihojiwa na askari wa kampuni binafsi ya ulinzi, kwa kuwa alikuwa amebaba mfuko na alipoulizwa kitu gani kabeba aliwajibu viatu,” ameeleza Muliro na kuongeza;


“Inadaiwa walipo mhoji alipaniki na kuanza kutokwa na jasho kabla ya kunyanyuka, waliokuwepo hawakujua anakwenda wapi na kumuona anatoka dirishani na kudondoka,” amesema Muliro.


Shuhuda

“Mimi nilisikia kitu kama mlio wakati nageuka naona bati limetoboka kwa juu, kuangalia vizuri nikaona binadamu chini kadondoka yupo chini ya meza, kuangalia kajirusha kutoka juu, kumbe ni dereva anayemuendesha bosi,” anasimulia Octa Chuwa, fundi viatu anayefanya kazi kando na jengo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad