Prof. Jay Afunguka "BASATA Sio Polisi, Soon Narejea"

Prof. Jay Afunguka "BASATA Sio Polisi, Soon Narejea"



Baraza la Sanaa tanzania (BASATA) limemtembelea msanii nguli wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay nyumbani kwake, Mbweni Dar es Salaam na kumjulia hali baada ya kuugua kwa takribani mwaka mzima.

Kupitia kurasa zake zake za mitandao ya Kijamii, Mbunge huyo wa zamani wa Mikumi kupitisha Chadema ameweka picha akiwa na Katibu Mtendaji Mkuu wa BASATA, Dkt. Kedmon Mapana na kuandiak ujumbe huu;

"Nilitembelewa na Katibu mtendaji mkuu wa BARAZA LA SANAA LA TAIFA @basata.tanzania, Dr. Kedmon Mapana @kmapana nyumbani kwangu Mbweni, tuliyajenga mengi sana kuhusu sanaa yetu hasa fungia fungia ya nyimbo za wasanii maana Baraza la sanaa ni walezi na sio polisi, pia nilimuahidi atanisikia tena hewani siku si nyingi STAY TUNED."

Hivi karibuni Prof. Jay alitembelewa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete na kumjulia hali.

Viongozi mbalimbali na mastaa wenzake wa muziki na filamu wameshamtembelea Prof. Jay mara baada ya kutoka katika Hospitali ya taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa muda mrefu akipatiwa matibabu kisha kuruhusiwa mabapo kwa sasa anaendelea vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad