Rais Samia Atoa Ufafanuzi: Mabadiliko ya Mawaziri na Makatibu sio Adhabu



Rais Samia Atoa Ufafanuzi: Mabadiliko ya Mawaziri na Makatibu sio Adhabu


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Viongozi wateule Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar leo September 01,2023 ambapo amesema mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu aliyoyafanya sio adhabu bali ni mabadiliko ya kawaida ya kuimarisha maeneo ya utendaji kazi.


Rais Samia amesema “Mlipoanza kuapa mmesema ‘Mimi fulani fulani naahidi umma kwamba nitakuwa Mzalendo n.k’, sasa kile kiapo mnaweza kuona mmeapa tu kwasababu Jaji Mwangesi anataka muape, hapana, ni kiapo ambacho hata Mungu anakisikia naomba mkatimize kiapo chenu”


“Mabadiliko haya ni adjustment , maendeleo lazima yawe na bandika bandua, kaza nati fungua, toa nati hii weka hapa ndio maana ya mabadiliko haya lakini tukikaa wenyewe (Kwenye kikao kazi) nitawaeleza kiundani”


“Kwa wale wapya Jerry Silaa na wengine nadhani mnayaona yanayotokea Bungeni na mmekuwa mkipaza sauti kubwa kwa Mawaziri sasa yale mliyokuwa mnapaza kwa Mawaziri mnakwenda kuyafanya nyinyi, wanasema ukitaka uhondo wa ngoma…? sasa mpo kwenye ngoma tunatarajia mcheze kwelikweli na mlete yale mabadiliko mliyokuwa mkiyahoji”


“Mabadiliko haya sio adhabu, ni mabadiliko ya kawaida ya kuimarisha maeneo yetu, natarajia commitment na utumishi, sisi ni Watumishi wa Watu sasa kuna mwingine akipata uteuzi anajiona eeh atanijua Mimi ni nani, sisi ni Watumishi wa Watu, katika utumishi mahusiano ni jambo zuri sana, ukijipandisha unataka kukaribia Mbinguni kwamba umepata uteuzi wewe nani wewe nani hutotumikia Watu”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad