Rais Samia "Hatujaruhusu Mikutano ya Siasa Watu Wakatukane"


Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Sept 11,2023 ameshiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia, Jijini Dar es salaam ambapo amevitaka Vyama kutumia mikutano hiyo kujijenga na sio kutukana, kutoa kashfa na kuchambua Dini za Watu.

Rais Samia amesema “Tumeruhusu mikutano ya hadhara ili Vyama vizungumze Wananchi wasikie sera zao ili Vyama vikue virudishe wale waliowapoteza tukienda kwenye Uchaguzi Vyama vimejipanga vya kutosha”

“Hatukutoa fursa ya mikutano ya Vyama vya Siasa ili Watu wakavunje sheria, wakasimame kutukana, wakasimame kukashfu, wakasimame kuchambua dini za Watu lakini sishangai kwanini haya yanatokea kwasababu ya kuzungumza hakuna”

“Tulianza oooh na Katiba ikaenda ikakatika katikati, ikaja ooh Bandari ikaenda ooh Katiba tena, hakuna na inapokuwa hakuna unalazimisha lazima ufanye jambo utazungumza lisilokuwepo”

“Niombe Vyama vya siasa tutumie fursa kujijenga kwa Wananchi, ili Wananchi wawaunge tena mkono tukienda kwenye uchaguzi Vyama vyote viwe vimejipanga”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad