Rais Samia: Tuheshimu Mipaka, Uhuru wa Maoni

Rais Samia: Tuheshimu Mipaka, Uhuru wa Maoni


Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuna uhuru wa maoni lakini una mipaka yake siyo tu kisheria hata kibinadamu.


Hayo ameyazungumza leo Jumatatu Septemba 10, 2023 katika Mkutano Maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa na wadau wa demokrasia amesema kuwa aliye muungwana anajua mipaka yake.


Samia amesema ana kikundi maalumu kinachoangalia maoni yote yanayotolewa na kuchukua yale mazuri na kuyafanyia kazi.


‘Kuna uhuru wa maoni lakini uhuru wa maoni una mipaka yake siyo tu kisheria hata kibinadamu, kama ulizaliwa ukalelewa vyema ukapitishwa kwenye masomo tunayosoma, lakini ukapitishwa kwenye masomo ya dini ukaielewa vizuri, kuna mambo huwezi kufanya tu, kama ulipata malezi mazuri ukaijua dini yako ukakua kwenye misingi mizuri kuna mambo huwezi kufanya.


“Utasikia mama una kifua una stahimili utafanyaje? Jamani kama mwendawazimu anachukua nguo zako anaenda mbio na wewe utoke utupu, umfukuze? Mwendawazimu ni yupi? Wengine tulilelewa kwenye maadili tukapitishwa kwenye dini huwezi kufanya hayo na mwengine kaumbwa hivyo roho yake basi tu raha yake aone ugomvi, mabishano na huyo amua leo, mimi nakupa Serikali na wenzio hao kwenye kikundi ataunda chama kingine awapinge wale wale wenzio aliokuwa nao.


“Na ndio tunayoyaona huko kwao, ukiona hawapo si tu kwamba kuna kununa hakukaliki huko ndani wengine twende wengine tusiende, sasa kwa tabia kama zile watakuwa na amani kweli?


Uhuru wa kutoa maoni una mipaka yake kama ulizaliwa na baba yako na mama ukalelewa vyema ukapitishwa kwenye mafunzo ya dini kuna meno mengine huwezi kusema,” amesema Rais Samia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad