Michael Emenalo Mkurugenzi wa Saudi Pro League amekana madai kwamba ligi ya Saudia itakabiliwa na hatima sawa na Ligi Kuu ya China, ambayo uwekezaji wake mkubwa katika miaka ya 2010 hatimaye ulimalizika baada ya miaka michache tu.
"Sio kwamba itadumu lakini naamini itabaki na itaendelea kukua,Kama kuna mtu ametilia maanani soka la Saudia, atajua kwamba watu wake wanaupenda sana mchezo huu huu , ni mpango uliowekwa vizuri ambao umekuwepo kwa muda mrefu sana “.
“Hatuleti wachezaji tu kuwalipa ili waweze kukimbia na kuwa maarufu kwa siku chache,Kuna mpango wa kuboresha miundombinu na kuendeleza academy, kuna mkakati mkubwa zaidi wa hilo. Sio ununuzi wa wachezaji pekee, ndio maana naamini ligi iko hapa kukaa kwa muda mrefu sana."