Sada Aliyetoroka Nyumbani Apatikana, Aliomba Kazi ya Housegirl na Kubadili jina, Mama asimulia



Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Sunshine iliyopo Kibaha Mkoani Pwani, Sada Kabaju (17) ambaye alitoroka nyumbani tangu August 18 baada ya kupigwa na Kaka yake kwa kosa la kujihamishia fedha kutoka kwenye simu ya Mama yake bila ruhusa, amepatikana akiwa Ubungo Msewe Dar es salaam anakodai aliomba kazi ya kuwa House Girl ili apate pesa ya kumlipa Mama yake.

Mama Mzazi wa wa Sada, Zaiba Kinyowa (58) ameiambia @AyoTV_ kupitia mahojiano yake na Mwandishi Bakari Chijumba kuwa Sada amesema alipotoka nyumbani alikaa Gesti kwa siku tatu na alipoishiwa fedha akaomba kazi ya kuwa House Girl kwa Mtu akidai anatokea Iringa na akabadilisha jina na kujiita Rachel pamoja na kujiongezea miaka na kusema ana umri wa miaka 19.

“Nimefurahi sana kumuona Mwanangu, nilipigiwa simu na Mtu usiku jana akaniambia amemuona Sada akasema namuona hapa Mtoto ni kama yule niliyeona picha yake kwa MillardAyo, nimemuona Mwanangu nikapiga kelele sana, Sada mwenyewe akawa ananibembeleza, tukaja nyumbani, Msamaria Mwema anasema alipomuona alimuuliza wewe ni Sada akakataa akamuonesha picha iliyopostiwa na MillardAyo bado akasema sio yeye kwamba yeye anaitwa Rachel”

“Sada anasema alitumwa kununua dawa ya mbu na alipofika dukani Msamari mwema akamuona, amesema wazo la kurudi hakuwa nalo alipanga akipokea mshahara anitumie tu hela na abaki hukohuko hakupanga kurudi nyumbani”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad