Sam Larry Afunguka Tuhuma za Kuhusuka na Kifo Cha Mwimbaji Mohabad



Promota Wa Muziki Na Rafiki Wa Karibu Wa Naira Marley #SamLarry Ameibuka Na Kutoa Taarifa Kuhusu Kuuawa Kwa Mohbad Ikiwa Nae Ni Mmoja Kati Ya Watuhumiwa Wa Kifo Cha Muimbaji Huyo.

#SamLarry Katika Taarifa Yake Amesema Kwamba Aliwahi Kumpa Mohbad Kiasi Cha N2M (Tsh Milioni 6.2/=) Kwa Ajili Ya Kutumbuiza Katika Mazishi Ya Mama Yake Mzazi Lakini Mohbad Hakutokea Kabisa Kwenye Sherehe Ya Kumbukumbu Ya Marehemu Mama Wa Sam Larry, Na Hata Alipodai Fedha Zake Mohbad Alisema Kwamba Alipoteza Simu Yake Pamoja Na Pesa Baada Ya Taasisi Ya Kupinga Matumizi Ya Dawa Za Kulevya Nigeria (NDLEA) Kumkata Nyumbani Kwake

Sam Larry Ameendelea Kusema Kwamba "Kuna Siku Nilisikia Kijana Huyu Huyu (Mohbad) Ana-Shoot Video Jirani Na Nyumbani Kwangu, Ikabidi Nimfuate Hadi Pale Kudai Fedha Zangu, Ila Tuliishia Kugombana/ Kutoelewana Kwa Zaidi Ya Dakika 5, Lakini Kuna Rafiki Yake Alisema Kwamba Atalipa Fedha Hizo Lakini Hadi Leo Sijalipwa Hata Cent. Ikabidi Tu Nipotezee Niendelee Na Mambo Yangu (Move On)"

Pia Sam Larry Amedai Kwamba Baada Ya Hapo Alisafiri Kwenda Kenya (Mwaka Huu 2023) Kwa Ajili Ya Kutafuta Msanii Mwingine Wa Kutumbuiza Katika Sherehe Ya Kumbukumbu Marehemu Mama Yake, Ambapo Tangu Agosti 20 Hakuwepo Nchini Nigeria Na Hivyo Hajui Chochote Kuhusu Mohbad Zaidi Ya Hizi Taarifa Kwenye Tovuti Mbalimbali Za Habari. "Nimerudi Nchini Kwa Furaha, Hivyo Sifahamu Chochote kuhusu Muimbaji Huyo Alivyofariki"

Sam Larry Alitua Nigeria Usiku Wa Kuamkia Leo Na Alikamatwa Na Jeshi La Polisi La Lagos Na Kuwekwa Chini Ya Ulinzi Kwa Ajili Ya Uchunguzi Wa Kifo Cha Mohbad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad