Mlinzi wa Yanga Joyce Lomalisa anaweza kurejea dimbani kabla ya mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh
Mchezo huo utapigwa Jumamosi ijayo, Septemba 30 2023 katika uwanja wa Azam Complex
Lomalisa alikuwa miongoni wa wachezaji walionyesha kiwango cha juu katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Rwanda na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Majeraha aliyopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc uliopigwa Jumatano iliyopita yalitishia hatma yake ya kushiriki mchezo wa marudiano
Hata hivyo kulingana na daktari wa Yanga, Moses Itutu amesema jeraha alilopata Lomalisa sio tishio na alipewa mapumziko ya siku tano mpaka saba
"Jeraha lake sio tishio, tuliona tumpe muda wa mapumziko ili aweze kupona vizuri zaidi na atakuwa nje kwa muda wa siku tano hadi saba," alisema Itutu
Lomalisa anaweza kurejea kikosini siku ya Jumanne na pengine kushiriki maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo dhidi ya Al Merrikh utakaopigwa Jumamosi