Idadi imethibitishwa na Afisa wa Ubalozi Mwandamizi wa Tanzania Nchini humo, Peter Shija baada ya kutembelea eneo la tukio ambapo pia amesema wengine 3 wako Hospitali baada ya kupata Majeraha
Imedaiwa kuwa Jengo hilo lililokuwa chini ya Umiliki wa Jiji la Johannesburg, lilitelekezwa na kuanza kutumiwa Watu waliokosa makazi, wengi wao wakiwa Wahamiaji wasio na vibali
Kwa mujibu wa Afisa Ubalozi huyo, zaidi ya Watanzania 150 walikuwa wakiishi ndani ya Jengo hilo kabla ya kuteketea kwa moto ambao umesababisha vifo vya Watu zaidi ya 74
-