TARURA waonywa uchimbaji mashimo barabarani

TARURA waonywa uchimbaji mashimo barabarani


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewataka watendaji wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini – TARURA, kuacha utaratibu wa kuchimba barabara na kuziacha na mashimo kwa muda mrefu bila kuyafukia.

Aidha, pia ameonya kuwa atawaondoa katika nafasi zao watendaji wa TARURA pamoja na Mameneja wa TARURA wa Mikoa na Wilaya pale ambapo mashimo hayo yataachwa wazi hadi wiki mbili bila kuyafukia kwa utaratibu unaofaa.

Hata hivyo, Waziri Mchengerwa amesema yapo mashimo yamechimbwa na kuachwa wazi kwa mwezi mzima, hali inayosababisha adha kwa watumiaji wa barabara na wakati mwingine kusababisha ajali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad