Tunapambania Kufuzu Wenzetu Tunaocheza Nao Wanafikiria Ubingwa


Tunapambania Kufuzu Wenzetu Tunaocheza Nao Wanafikiria Ubingwa


Tunakutana na Algeria ambayo tayari imeshafuzu kucheza Fainali za AFCON nchini Ivory Coast, sisi [Tanzania] bado tunapambana kutafuta walau alama moja ambayo itatuvusha kwenda kwenye Fainali za AFCON.


Ukiangalia ubora wa Algeria na Tanzania wenzetu wapo mbali sana, wakati sisi tunapambana kufuzu wao wanaweka mipango ni namna gani wataweza kufanya vizuri na kushinda ubingwa wenyewe.


Kitu pekee kitakachotufanya tufanikiwe leo ni mipango na mbinu za Kocha [Adel Amrouche] kwa sababu ukiangalia ubora wa mchezaji mmoja mmoja na ubora wa timu wenzetu wapo mbali sana.


Kwa hiyo kitu cha msingi kwa Kocha kuangalia ni aina gani ya mbinu za kutumia ili kupata tunachokitaka.


- Master Tindwa, Mchambuzi Clouds Media.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad