Kocha wa Uganda, Milutin Sledjovic Micho ametoa shutuma kwa Algeria na Tanzania kuwa ni kama walipanga kutoka sare kwenye mchezo wao uliopigwa dimba la Annaba uliofanikisha Tanzania kufuzu AFCON
Micho anadai kuwa ni kama Algeria walipanga na Tanzania kufanya hivyo ili kuirahisishia Taifa Stars kufuzu na wao kuangukia pua licha ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Niger
Kocha huyo ameomba Algeria na Tanzania kutolea ufafanuzi suala hili na abainike aliyehusika na suala zima
Aidha aliongeza kuwa kila mmoja anatambua DNA ya kocha wa Algeria, Djamel Belmadi katika suala zima la kusaka ushindi hivyo haamini kama Tanzania walipata sare kwa uwezo
Tanzania iliungana na Algeria kufuzu michuano ya Afcon 2023 baada ya kumaliza nafasi ya pili kundi F ikiwa na alama nane
Uganda walimaliza nafasi ya tatu wakiwa na alama saba. Ni wazi malalamiko ya Micho ni baada ya timu yake kukosa nafasi lakini kwa wlaiofuatilia mchezo kati ya Algeria na Tanzania wanafahamu ni kwa kiasi gani mchezo huo ulikuwa mgumu na vile wachezaji wa Tanzania walipambana uwanjani, walistahili alama moja ambayo ilitosha kuwapeleka Afcon 2023