Unaambiwa Power Dynamos Walificha Silaha zao Walivyokuja Simba Day

 

Unaambiwa Power Dynamos Walificha Silaha zao Walivyokuja Simba Day

Shabiki wa Klabu ya Simba, Aggy Danny maarufu kama Aggy Simba, amesema kuwa wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa frika, Power Dynamos ya Zambia walificha baadhi ya wachezaji wao kwenye mchezo waliowaalika wakati wa sherehe za Simba Day, mwezi Agosti mwaka huu kwenye Dimba la Mkapa.


Simba wameanza safari leo kuelekea Zambia kuwafuata Power Dynamos kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa kwenye Dimba a Levy Mwanawasa, wakati Simba wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga timu hiyo bao 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki wa SImba Day.


Aggy amesema kuwa, Simba imejiandaa vyema kwa ajili ya kwenda kupata ushindi ugenini ili kujihakikishia kusonga mbele katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.


"Tutaenda kukutana na Power Dynamos ambayo tumecheza nao kwenye Simba Day, wakati wanakuja Simba Day walikuwa wanajua kabisa wanaenda kwenye Champions League watacheza na timu fulani wakitoka watakutana na Simba.


"Kwa hiyo inawezekana pia walivyokuja hapa kwa Mkapa labda hawakutaka kujionesha wao wako vipi.


"Wanaweza wakawa walicheza wakaficha silaha zao ili kutuonesha kwamba wao ni wa kawaida kwa sababu walikuwa na imani kubwa maybe wangekutana na Simba (kwenye Champions League), hivyo hatuwezi kusema sana kwamba watakuwa ni wa namna gani," amesema Aggy Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad