Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya
uteuzi wa viongozi mbalimbali leo.
a) Uteuzi wa Katibu Mkuu
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amemteua Balozi Stephen Patrick Mbundi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
Balozi Mbundi atachukua nafasi ya Balozi Prof. Kennedy Godfrey Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
b) Uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu
Amemteua Balozi Said Shaib Mussa – Balozi wa Tanzania, Kuwait kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.Balozi Mussa anachukua nafasi ya Balozi Fatma Rajab ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania, Qatar.
c) Uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Amemteua Balozi Prof. Kennedy Godfrey Gastorn kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Balozi Prof. Gastorn anachukua nafasi ya Dkt. Evaristo Longopa ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
d) Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani
i) Amemteua Mhe. Jaji Lameck Michael Mlacha kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi Jaji Mlacha alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kigoma.
ii) Amemteua Mhe. Jaji Paul Joel Ngwembe kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi Jaji Ngwembe alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Morogoro.
iii) Amemteua Jaji Mustafa Kambona Ismail kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi Jaji Ismail alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu, Dar es Salaam.
iv) Amemteua Jaji Abdul-Hakim Ameir Issa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi Jaji Issa alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Zanzibar.
e) Uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu
i) Amemteua Dkt. Evaristo Longopa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Dkt. Longopa alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
ii) Amemteua Bw. Wilbert Martin Chuma kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bw. Chuma alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Rufani Dar es Salaam.
iii) Amemteua Bi. Sharmillah Said Sarwat kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bi. Sarwat alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
iv) Amemteua Bw. Arnold John Kirekiano kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bw. Kirekiano alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
v) Amemteua Bi. Martha Boniface Mpaze kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bi. Mpaze alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Jumuishi katika Masuala ya Mirathi na Familia, Dar es Salaam.
vi) Amemteua Bw. Ferdinand Hilali Kiwonde kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.Kabla ya uteuzi Bw. Kiwonde alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu.
vii) Amemteua Bw. Said Rashid Ding’ohi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bw. Ding’ohi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Iringa.
viii) Amemteua Dkt. Angelo Kataraiya Rumisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Dkt. Rumisha alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
ix) Amemteua Bi. Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.
x) Amemteua Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bw. Mwakahesya alikuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri, Ofisi ya Rais Ikulu, Dodoma.
xi) Amemteua Bw. Griffin Venance Mwakapeje kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.Kabla ya uteuzi Bw. Mwakapeje alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Wizara ya Katiba na Sheria, Dodoma.
xii) Amemteua Dkt. Dafina Daniel Ndumbaro kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.Kabla ya uteuzi Dkt. Ndumbaro alikuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dodoma.
xiii) Amemteua Bw. Emmanuel Ludovick Kawishe kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bw. Kawishe alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dodoma.
xiv) Amemteua Bw. Abdallah Halfan Gonzi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.Kabla ya uteuzi Bw. Gonzi alikuwa Mjumbe wa Baraza la Rufani za Kodi (TRAT) na Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
xv) Amemteua Bw. Kamazima Kafanabo Idd kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.Kabla ya uteuzi Bw. Idd alikuwa Mhadhiri Msaidizi Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam.
xvi) Amemteua Bw. Frank Muyoba Mirindo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bw. Mirindo alikuwa Mhadhiri Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Tanga.
xvii) Amemteua Bi Hadija Ally Kinyaka kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bi. Kinyaka alikuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili ya Lawhill Co. & Advocates, Dar es Salaam.
xviii) Amemteua Bi. Aisha Ally Sinde kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bi. Sinde alikuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili BOWMANS Tanzania, Dar es Salaam.
xix) Amemteua Bw. Hussein Salum Mtembwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.Kabla ya uteuzi Bw. Mtembwa alikuwa Wakili wa Kujitegemea na Mmiliki wa Kampuni ya Uwakili ya HM Noble Attorneys, Mtwara.
xx) Amemteua Bi. Irene Daniel Musokwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya uteuzi Bi. Musokwa alikuwa Wakili wa Kujitegemea na Mshiriki katika Kampuni ya Uwakili ya FC Attorneys, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 3, 2023 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imefafanua kuwa, uteuzi huu ni kuanzia Septemba 3, 2023.