Wabunge wagoma Trevor Noah kulipwa bilioni 4.2 kwa video ya dakika 5 ya kutangaza Utalii



Pendekezo la kumlipa Trevor Noah Randi Milioni 33 sawa na takriban Tsh. Bilioni 4.2 kwa Video ya Dakika 5 ili kuitangaza South Africa kama Kivutio cha Kitalii, limesababisha mpasuko baada ya baadhi ya Wabunge na Wananchi kupinga kwa kudai kuwa Nchi hiyo inapitia Mgogoro mkubwa wa kifedha kwa wakati huu.


Akitoa pendekezo hilo, Waziri wa Utalii, Patricia de Lille amesema kuwa Mcheshi na Mtangazaji huyo atalipwa na Baraza la Biashara la Utalii nchini humo (Shirika Mwamvuli linalowakilisha wadau wa Usafiri na Utalii wa Nchi hiyo), na sio kwa fedha za Umma.


Hata hivyo, wadau wengine wameunga mkono pendekezo hilo wakisema ushawishi wa Nyota huyo unaweza kukuza Utalii wa Afrika Kusini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad