Walimu Waonywa Kuhusu Mikopo 'Kausha Damu'

 

Walimu Waonywa Kuhusu Mikopo 'Kausha Damu'

Walimu katika wilaya za Kasulu na Buhigwe mkoani Kigoma wametakiwa kujihadhari na taasisi zinazotoa mikopo isiyozingatia sheria na sera za mikopo za Benki Kuu (BoT), zikiwa na riba kubwa ambazo zimeathiri maisha na utendaji kazi wa walimu.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu,Dolla Kusenge ametoa rai hiyo akifungua kongamano la Siku ya Mwalimu lililoandaliwa na Benki ya NMB na kushirikisha walimu zaidi ya 200 kutoka kwenye wilaya hizo.


Amewataka walimu kuachana na mikopo hiyo inayojulikana kama ‘Mikopo Umiza’ au Kausha damu, kwani inawaumiza, badala yake wametakiwa kutumia benki rasmi zinazotambuliwa na serikali ikiwemo NMB, ambazo zimekuwa zikitoa huduma na mikopo ambayo imeboresha maisha ya walimu.


Akizungumzia kongamano hilo, Meneja wa Kanda ya Magharibi wa benki ya NMB, Vicent Urio amesema limeandaliwa maalum kwa ajili ya kupata mrejesho wa walimu kuhusiana na huduma kwa walimu maarufu kama Mwalim Spesho zilivyowezesha kuwafikia walimu na changamoto zilizojitokeza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad