Takriban Watahiniwa 49,948 kati ya 102,948 waliotarajiwa kufanya Mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi Mkoani Kigoma, hawajafanya Mtihani huo unaotarajiwa kumalizika nchini kote leo Septemba 14, 2023
Kwa mujibu wa Afisa Elimu wa Mkoa, Paulina Ndigeza amesema Wanafunzi wengi hawakuweza kufanya Mtihani huo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo utoro na mwamko mdogo wa Wazazi katika kuwasimamia Watoto wao.
Aidha, kwa mujibu wa ripoti ya CAG ya mwaka 2021/22 ni kuwa Shule za Msingi nchini ziliripotiwa kuwa na upungufu wa Madawati 158,066, Vyoo vya Wanafunzi 56,530 na Nyumba za Walimu 35,684.
Mapungufu mengine ni pamoja na Viti na Meza 29,829, Madarasa, 27,316, Ofisi za Walimu 2,266 na Vyoo vya Walimu 622.