Wanawake Misri wauawa kwa kuwakataa wanaume




Mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Cairo ameuawa kwa kupigwa risasi kwenye eneo la chuo na aliyekuwa mfanyakazi mwenzake aliyejulikana kwa jina la Ahmed, wizara ya mambo ya ndani ilisema, katika kisa cha hivi karibuni cha mauaji ya wanawake nchini Misri.

Mshukiwa huyo baadaye alifuatiliwa katika eneo la Matrouh, magharibi mwa mji mkuu, ambako "alijiua kwa kujipiga risasi kwa silaha ile ile" iliyotumiwa katika mauaji ya mwamamke huyo ambaye pia alijulikana kwa jina lake la kwanza la Nurhan.

Gazeti la serikali la Al-Ahram lilisema mwanamke huyo, Nurhan, alikataa ombi la kuolewa na Ahmed, ambaye alikuwa akimsumbua mara kwa mara.

Mtu huyo aliyekuwa na silaha aliwahi kukamatwa, baada ya "kulichoma moto gari la muathirika miaka mitano iliyopita na kufanya vitisho kwa kumtumia ujumbe mfupi," gazeti hilo la Al-Ahram liliongeza.


Siku moja kabla, vyombo vya habari vya ndani vilisema mwanamke mmoja alipigwa risasi na kufa siku ya Jumanne na mchumba wake wa zamani wakati akitoka kazini katika wilaya ya Heliopolis huko Cairo.

Nchi hiyo ya kiconservative ya Afrika Kaskazini imeshuhudia msururu wa mauaji ambayo yamezua hasira na hofu ya kuenea ghasia.

Mwezi Juni 2022, Nayera Ashraf aliuawa kwa kuchomwa kisu mbele ya chuo kikuu alichokuwa akisoma huko Mansoura, kaskazini mwa Cairo, baada ya kukataa maombi ya mwanafunzi mwenzake Mohamed Adel.


Video ya shambulio hilo ilisambaa, na Adel baadaye alihukumiwa kifo na kunyongwa mwezi Juni.

Mwanamke mwingine, Kholood al-Sayed mwenye umri wa miaka 21, aliuawa nyumbani kwake kaskazini mwa mji wa Port Said na mchumba wake mwaka 2022 baada ya kujaribu kumkimbia , kulingana na waendesha mashtaka.

Mwezi Agosti mwaka 2022, mwanafunzi aliyejulikana kama Salma aliuawa huko Zagazig, kaskazini mwa mji mkuu, na mwanamume aliyemkataa yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad