Kanuni za kibiashara zinawakataa Juma Jux, Ommy Dimpoz, Young Lunya, Marioo, Chege, Rayvanny, Whozu na wengineo wengi kupata malipo bora ndani ya Wasafi Festival.
Tayari wao walishaonesha mara nyingi kuwa wapo chini ya Diamond, kwa kila kitu. Tayari wasanii hao tajwa hapo juu wamepeleka maombi ya kufanya wimbo na Diamond.
Wasanii wote tajwa hapo juu wanafukuzia au wana ndoto ya kufanya wimbo na Diamond.
Tayari wamekubali wao wapo chini ya Diamond. Mbaya zaidi wengi wana mahusiano hadi na wanawake waliotembea na Diamond, wakiamini watapata umaarufu kama Diamond kupitia mapenzi.
Kupitia kanuni za kibiashara inaonesha Wasafi Festival ilikuwa inaweza kufanyika na Wasanii wa WCB tu na watu wakaja. Swali la msingi je wasanii tajwa hapo juu wanaweza kufanya muziki bila Diamond?
Jibu hapana katika Meza ya Diamond kumejaa maombi ya wasanii kufanya wimbo na yeye. Wapo wasanii ambao wana taka kufanya wimbo na Zuchu, Lavalava na Mbosso.
Kama wangelikuwa na msimamo wa kimuziki kama Alikiba wangelipwa fedha nzuri, walihitaji nusu ya msimamo wa Alikiba ili kulipwa fedha nzuri.
Walihitaji nidhamu ya fedha na kutunza wanachopata ili wasiwe watumwa wa msanii mwenzao. Walihitaji nusu ya nidhamu ya Alikiba katika fedha ili wawe na msimamo wa kifedha.
Bahati mbaya fedha zao nyingi hutumia kuishi maisha ya Mitandaoni na kuigiza. Hupanga nyumba za gharama kubwa na kufanya safari nyingi za nje ili waonekane matajiri.
Wanastahili laki tano sababu nao wanahitaji msaada kutoka kwa Diamond. Tuendelee na na wimbo mpya Huku, huku kila mmoja akiwaza anataka kushikwa wapi?