Yanga Imekuwa TIMU ya 3 Kwa Ubora Afrika, Fahamu Vigezo Vilivyotumika
Shirikisho la kimataifa la kutunza Takwimu na Historia za mpira Duniani ‘IFFHS’ limetoa Orodha ya Timu 10 bora barani Afrika kwa mwaka mzima (kuanzia Septemba 1, 2022- Agosti 31, 2023).
Yanga imeshika nafasi ya 3 nyuma ya Al-Ahly na Wydad Casablanca.
Duniani Yanga ipo nafasi ya 63, juu ya Chelsea (72).
Vigezo vilivyotumika;
Al Ahly Cairo — 01
Champions league - Bingwa
Premier league - Bingwa
Wydad Casablanca — 02
Champions league - Fainali
Premier league - mshindi wa pili
Young Africans — 03
Premier league - Bingwa
Confederations cup - Fainali
FA cup - Bingwa
Pyramids — 04
Premier league - Mshindi wa pili
Confederation cup - Nusu fainali
Mamelodi Sundowns — 05
Premier league - Bingwa
Champions league - Nusu fainali
FAR Rabat — 06
Premier league - Bingwa
Confederation cup - Nusu fainali
Raja Casablanca — 07
Champions league - Nusu fainali
FA cup - Fainali
Zamalek — 08
Premier league - Mshindi wa pili
Champions league - 16 bora
FA cup - Bingwa
CR Belouzdad — 09
Premier league - Bingwa
Champions league - Nusu fainali
USM Alger — 10
Confederations cup - Bingwa
Kwa mujibu wa shirika hilo lenye makazi yake Nchini Switzerland hutoa alama kwa kuzingatia mashindano yote.
◉ Champions league
◉ Confederations cup
◉ Premier league
◉ FA cup.
Timu zilizofanya vizuri kwenye mashindano hayo kwa ujumla (sio shindano moja pekee) hu-score points nyingi zaidi. Pia ubora wa ligi husika huchangia alama kwa timu.
Kwa nini USM Alger amechukua kombe halafu akazidiwa na Yanga? Ni kwa kuwa kwenye mashindano mengine kama ligi kuu (8) & FA hakufanya vizuri, ndiyo maana amezidiwa.
Rank zimepangwa kwa kuzingatia alama zilizokusanywa kwa mwaka 1, kuanzia 1 Septemba 2022 hadi 31 Agosti 2023.
Unafiki unakuja vipi?
Hawa IFFHS walivyotoa takwimu hapo nyuma walisifiwa sana na baadhi ya wachambuzi na mashabiki, cha ajabu wachambuzi walewale waliozisifu takwimu zao wakati ule leo hii wanazikosoa.