Aidha msimu uliopita Wananchi wakapiga hatua kubwa kwenye michuano ya Kimataifa wakifanikiwa kucheza fainali ya kombe la Shirikisho CAF CC wakimaliza katika nafasi ya pili
Haishangazi kuona Yanga imeendelea kupaa kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa na taasisi mbalimbali
Kwa mujibu wa shirika la tafiti na habari Duniani la IFFHS limeitaja klabu ya Yanga kuwa klabu namba tatu (3) barani Afrika ikiwa nyuma ya Al Ahly na Wydad Casablanca. Hizi ni takwimu za kuanzia Septemba 2022 hadi Augsut 2023
Takwimu hizi zinahusisha mashindano yote yaani ligi ya ndani ya mechi za Kimataifa
IFFHS ni Shirika linalotambuliwa na FIFA, limekuwa likitoa takwimu mbalimbali za michezo. Ni shirika hili lililotoa takwimu juu ya ubora wa ligi na kuitaja Tanzania kushika nafasi ya tano kwa ubora wa ligi barani Afrika