Yanga ni Noma, Ni Mwendo wa Kuvunja Rekodi tu Africa



Katka kipindi cha misimu miwili mfululizo Yanga imetawala soka la ndani kwa kushinda mataji yote


Aidha msimu uliopita Wananchi wakapiga hatua kubwa kwenye michuano ya Kimataifa wakifanikiwa kucheza fainali ya kombe la Shirikisho CAF CC wakimaliza katika nafasi ya pili

Haishangazi kuona Yanga imeendelea kupaa kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa na taasisi mbalimbali

Kwa mujibu wa shirika la tafiti na habari Duniani la IFFHS limeitaja klabu ya Yanga kuwa klabu namba tatu (3) barani Afrika ikiwa nyuma ya Al Ahly na Wydad Casablanca. Hizi ni takwimu za kuanzia Septemba 2022 hadi Augsut 2023


Takwimu hizi zinahusisha mashindano yote yaani ligi ya ndani ya mechi za Kimataifa

IFFHS ni Shirika linalotambuliwa na FIFA, limekuwa likitoa takwimu mbalimbali za michezo. Ni shirika hili lililotoa takwimu juu ya ubora wa ligi na kuitaja Tanzania kushika nafasi ya tano kwa ubora wa ligi barani Afrika

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad