Yanga Wafunguka Mashabiki Kushindwa Kuangalia Mechi Rwanda

 

Yanga Wafunguka Mashabiki Kushindwa Kuangalia Mechi Rwanda

Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema, mashabiki wote watakaosafiri na mabasi kwenda Rwanda kwa ajili yua mchezo wao wa Klabu Bingwa dhidi ya Al Merrikh, wataingia uwanjani kushuhudia mtanange huo.


Kamwe ametoa kauli hiyo leo Septemba 12, 2023 kufuatia kuwepo kwa taarifa za chini chini za kwamba huwenda wapinzani wao wakawapa tiketi chache hivyo mashabiki wa Yanga kushindwa kuingia uwanjani.


"Hizi taarifa zimeibuliwa na watu wanaopenda kupelekwa mjini na sisi tumesema safari hii hatumpeleki mtu mjini. Yanga inaongozwa na viongozi makini wenye weledi, tumeshafanya mawasiliano na wenzetu kule Shirikisho la Mpira Rwanda na kila kitu kipo sawa, mashabiki wasiwe na hofu," alisema Kamwe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad