Yanga Yaitembezea Kichapo Al Merrikh, Yaweka Heshima Kubwa Rwanda

 

Yanga Yaitembezea Kichapo Al Merrikh, Yaweka Heshima Kubwa Rwanda

 Yanga Yaitembezea Kichapo Al Merrikh, Yaweka Heshima Kubwa Rwanda

Yanga ni kama imetanguliza mguu mmoja hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Al Merrikh.


Mchezo huo wa mkondo wa kwanza hatua ya mtoano umepigwa katika Uwanja wa Kigali Pele nchini Rwanda.


Yanga wameibuka na ushindi huo huku kwa mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Kennedy Musonda alieingia kutokea benchi akimaliza krosi safi ya Pacome Zouzua na Clement Mzize aliefunga bao la pili akipokea pasi ya kisigino kutoka kwa Aziz KI.


Yanga inahitaji angalau sare katika mchezo wa mkondo wa pili ili kukata tiketi ya kutinga hatua ya Makundi ambayo wana zaidi ya miaka 20 hawajatinga katika hatua hiyo.


Je unadhani Merrikh watapindua meza mchezo wa marudiano? tupe maoni yako

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad