Zuchu Amtwanga na Mic Shabiki......



Unaambiwa Zuchu ni kama rapa Cardi B tu, hawa watu hawataki utani wakiwa stejini kwenye kazi zao ukiwaletea za kuleta maiki inageuka silaha!


Iko hivi, Zuchu akiwa kwenye shoo ya marudio ya Wasafi Festival iliyofanyika jana Septemba 3, 2023 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, shabiki alimshikashika miguuni ndio mrembo huyo uvumilivu ulipomshinda.


Zuchu alimkumbusha shabiki kitu kinachoitwa 'mipaka' kwa kumtandika na mic moja chap kisha akaendelea na shoo yake kama hakuna kilichotokea vile.


Shoo hiyo ilirudiwa jana baada ya juzi kutokea hitilafu ya umeme na baadhi ya wasanii akiwmo Diamond kushindwa kupafomu ndipo ilipotangazwa shoo ya bure kufidia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad