No title




Zuchu anadai kuwa ni Diamond pekee ndiye mwanaume ambaye amewahi kuwa naye kimapenzi. Kweli? Hii ni ngumu kuamini lakini, ndio maneno ya hitmaker huyo wa Naringa alipokuwa akiulizwa maswali ya papo kwa papo na Mtangazaji wa Wasafi FM, Mchaga OG.


“Mpaka sasa ni wanaume na wanawake wangapi umeshawahi kulala nao kimapenzi,” Zuchu alilisoma swali hilo kwenye kikaratasi baada ya kutoa mguno wa mshangao.

“Mmoja,” alijibu kwa kicheko na kumkumbatia ‘baby’ wake Diamond aliyekuwa naye nje ya chumba cha hoteli waliyofikia huko Ruangwa wikiendi hii huku akimsindikiza na busu zito shavuni.

“Peke yake,” anaongeza huku Mchaga akimuongeza swali, “Hakuna mwingine?”

“Hayupo,” anajibu Zuchu. “We unamjua boyfriend wangu gani kwenye industry ndani ya nje! Hilo swali mngemuuliza yeye sasa.”

Kwa upande wake Diamond alijibu swali hilo kwa utani,”Mimi sijawahi kutembea na mwanamke mwingine, ndio wa kwanza huyu,” na kuingia chumbani!

Diamond orodha yake tunaijua, ila kwa Zuchu, pamoja na kutowahi kumfahamu mpenzi wake kabla ya kuanzisha uhusiano na Dangote, unaamini kuwa ndiye mwanaume wake wa kwanza?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad