Ajali ya Lori yaua Mtoto wa Mchungaji na Mzee wa Kanisa

 

Ajali ya Lori yaua Mtoto wa Mchungaji na Mzee wa Kanisa

Watu wawili wamefariki dunia hii leo kufuatia ajali ya lori namba T 644 AJC Mercedes Benz mali ya kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Mbozi, baada ya kupinduka katika mteremko wa Isalalo barabara ya Mbozi Msangano baada kufeli breki.


Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Theopista Mallya, amewataja waliofariki kuwa ni Levy Simkoko (30) aliyekuwa mzee wa kanisa kutoka Ushirika wa Mbuga na Hosiana Gavu (21)ambaye ni mtoto wa mchungaji.


Kamanda Theopista amesema chanzo cha ajali ni kutokana na kutokea hitilafu kwenye mfumo wa breki na baadaye ya kupasuka bomba mbili za upepo hali iliyosababisha gari kwenda kwa kasi na juhudi za dereva zikashindikana kisha likaanguka na kupinduka na kusababisha vifo vya watu viwili na majeruhi wawili ambao wametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.


Kamanda amesema kuwa hilo lori lilikuwa na watu 12 ambao walikuwa wanamsindikiza mchungaji Emmanuel Gavu aliyehamishwa kutoka ushirika wa Mbuga kwenda ushirika wa Msangano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad