AL AHLY Waanza Amafia, Watuma Majasusi Kibao Bongo Kuipeleleza Simba

 

AL AHLY Waanza Amafia, Watuma Majasusi Kibao Bongo Kuipeleleza Simba

AL AHLY Waanza Amafia, Watuma Majasusi Kibao Bongo Kuipeleleza Simba 

Imefahamika kuwa baadhi ya viongozi wa klabu ya Al Ahly ya Misri tayari wapo nchini Tanzania kwa ajili ya kuandaa mazingira ya ushindi kuelekea mchezo wao wa African Football League dhidi ya Simba SC.

Mchezo huo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali utapigwa Jumapili (Oktoba 20), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo wa ufunguzi unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’, Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ na wale wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa ambazo zimepatikana jijini Dar es salaam, ni kuwa tayari Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Tariq Hassani yupo jijini humo kwa ajili ya kutafuta moja ya Hotel ya nyota tano watakayofikia.

Pia Kiongozi huyo ameongozana na msafara wa watu 20 ambao wana majukumu mengine ya kuandaa mikakati ya kuhakikisha timu yao itakapokuwa jijini Dar es salaam haipati changamoto zozote.

Baadhi yao wanadaiwa kuifuatilia Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Fountain Gate, uliopigwa jana Uwanja wa Liti mkoani Singida, na Mnyama kuibuka na ushindi wa 2-1.

Kuhusu ujio wa maafisa hao wa Al Ahly jijini Dar es salaam, Meneja Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema: “Kama uongozi nguvu zetu zilikuwa zimeelezwa katika mchezo wetu wa jana, kama wenzetu wameanza kuwasili jijini Dar es salaam ni jambo zuri.

“Tumemaliza mchezo wetu Singida na sasa tunaanza kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly, kwa hiyo tutajipanga sisi kama sisi, ujio wao hautuhusu.

Share this:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad