Aliyetangazwa Kupotea Mazingira ya Kutatanisha Apatikana MOI, Aligongwa na Mwendokasi

 

Aliyetangazwa Kupotea Mazingira ya Kutatanisha Apatikana MOI, Aligongwa na Mwendokasi

 Aliyetangazwa Kupotea Mazingira ya Kutatanisha Apatikana MOI, Aligongwa na Mwendokasi

Siku chache baada ya kuwapo taarifa kwenye mitandao mbalimbali za kutoonekana kwa mfanyakazi wa hoteli ya Johari Rotana, Reuben Emmanuel Shilla (33) Mkazi wa Goba Mpakani jijini Dar es salaam, hatimaye amepatikana akiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi) baada ya kupata ajali kwa kugongwa na ‘mwendokasi’.


Taarifa za kutoonekana kwa Shilla zilianza kusambaa juzi Oktoba 16, 2023 baada ya jitihada za kumtafuta maeneo mbalimbali kutozaa matunda.


Akizungumza na Mwananchi Mkuu wa idara ya ulinzi katika hoteli ya Johari Rotana Theodory Stanley alisema Shilla hakuanza kuonekana tangu Jumapili October 15, alipoondoka kazini.


Meneja Mawasiliano MOI Patrick Mvungi, amethibitisha kupokelewa kwa mgonjwa huyo huku akieleza kuwa kutokana na changamoto aliyopata haruhusiwi kuzungumza.


Alipotafutwa kaka wa Shilla, hakuwa tayari kuzungumza badala yake alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno kuwa anamuhudumia mgonjwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad