Amri Kiemba "Azam Wakitaka Ushindi Leo Wapambane Kimaarifa na sio Kupania"

Amri Kiemba "Azam Wakitaka Ushindi Leo Wapambane Kimaarifa na sio Kupania"


Ukiangalia kikosi cha Azam FC huoni kama kuna unyonge utajitokeza dhidi ya Yanga, tofauti ambayo mimi huwa naiona Azam ikicheza dhidi ya Simba au Yanga, wachezaji wa Azam huwa wanapambana kama wamejaa sumu ‘wanacheza kama wana hasira’ hawa-enjoy kucheza.

Kwa daraja ambalo Azam FC imelitengeneza, wakicheza dhidi ya Simba au Yanga hawapaswi kuonekana kama JKT Tanzania au Ihefu kwa maana ya kwamba wao wanakuwa timu ya pili uwanjani wanapambana kwa jasho na damu matokeo yake maarifa yanapungua wanafanya makosa ya kawaida.

Natarajia kuwaona Azam wanapambana kwa maarifa na sio kupania hadi mwisho wa siku inakuwa vurugu na ndio maana huwa yanatokea makosa kutokana na kupoteza umakini yanayotokana na kupania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad