Bosi Simba: Sio Kinyonge, Tutamalizana Kwao Misri




AHMED Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, amesema hawatawafuata wapinzani wao Al Ahly kinyonge bali wanakwenda kifua mbele wakiamini watafanya maajabu ugenini.

Kuelekea kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya pili ya Africa Football League, Simba inahitaji ushindi kusonga mbele baada ya kushuhudia ubao ukisoma Simba 2-2 Al Ahly, robo fainali ya kwanza iliyochezwa juzi Ijumaa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ally alisema wakubwa hawana hofu ya kucheza mechi kubwa ugenini ama nyumbani, wanachotafuta ni ushindi.

“Hakuna asiyetambua ukubwa wa Simba ndio maana tupo kwenye timu 8 kubwa Afrika, kushindwa kupata ushindi hapa tunakwenda kuwafuata hukohuko kumalizana nao Misri.

“Sio kinyonge tena bali kazi yetu kubwa ni kutafuta ushindi kwenye mchezo wa robo fainali ya ugenini. Haitakuwa kazi nyepesi, lakini hatuna hofu tunajiamini na tunakwenda kufanya kweli.

“Mashabiki ni muda wa kuendelea kutamba kutokana na hatua ambayo tupo, wachezaji wanajituma nadhani mliwaona akina Kibu Denis, Jean Baleke, Saidi Ntibazonkiza akina Clatous Chama walivyokuwa wakitoa burudani,” alisema Ally.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad