Bosi Wa Tanapa Mwakilema Ateuliwa Kumrithi Jokate Wilaya Ya Korogwe


Bosi Wa Tanapa Mwakilema Ateuliwa Kumrithi Jokate Wilaya Ya Korogwe

Aliyekuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), William Simon Mwakilema.

Rais Samia Hassan leo Oktoba 3, 2023 amemteua William Simon Mwakilema, Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.


Mwakilema anachukua nafasi ya Jokate Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)


Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Aidha, Elibariki Bajuta, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora badala ya Kenan Laban Kihongosi ambaye amehamishiwa Momba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad