BREAKING: Kamanda Mkuu wa Hamas Auawa Katika Mashambulizi ya Anga ya Israel



BREAKING NEWS: Kamanda mkuu wa Hamas ameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) amesema.

Katika chapisho kwenye X, iliyoandikwa kwa Kiarabu, Avichay Adraee alisema Murad Abu Murad alihusika pakubwa katika shambulio la Israel Jumamosi iliyopita, ambalo liliua zaidi ya watu 1,300.

Hamas haijathibitisha kifo hicho.

Israel na Misri zasema raia wa Marekani huenda wakaondoka Gaza

Raia wa Marekani wataweza kuondoka Gaza kupitia mpaka wa Rafah kuelekea Misri, afisa wa Marekani anasema.

Kivuko hicho kitafunguliwa kuanzia saa 12:00 hadi 17:00 kwa saa za huko leo, kufuatia makubaliano kati ya serikali ya Israel na Misri.

Bado haijabainika iwapo Hamas, ambayo inadhibiti Gaza, itawaruhusu raia wa Marekani kuondoka katika eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad