BREAKING : Watu Mia Tano Wahofiwa Kufa Baada ya Bomu Kipigwa Hospitalini Gaza


Idadi ya watu waliouawa imefikia 500 kufuatia madai ya shambulizi la anga dhidi ya hospitali - kulingana na msemaji wa wizara ya afya ya Gaza.

Wakati huo huo, msemaji wa jeshi la Israel anasema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na jeshi linachunguza undani wake.

Tayari picha zinazotoka katika hospitali ya Al Ahli Arab zinaonyesha matukio ya kutisha - huku watu waliojeruhiwa wakitolewa nje kwa machela gizani.

Miili na magari yaliyoharibiwa yanaonekana yakiwa kwenye barabara iliyojaa vifusi.

Video ambazo hazijathibitishwa zilionekana kuonyesha mlipuko mkubwa muda mfupi kabla.

Mamia ya watu waliokimbia makazi yao walikuwa wamejihifadhi katika ukumbi kwenye uwanja wa hospitali, kulingana na wenyeji.

Maafisa wa ulinzi wa raia wanasema mlipuko huo ulitokana na shambulizi la anga la Israel na kwamba mamia wamenasa kwenye vifusi.

Jeshi la Israel linasema linachunguza tukio hilo.
Daktari ambaye jina lake halikutajwa anayefanya kazi katika hospitali hiyo ambayo imeshambuliwa katikati mwa Gaza.

Ameongeza kuwa kulikuwa na uharibifu mkubwa katika eneo la shambulizi - ambapo watu 4,000 waliokimbia makazi walikuwa wakitafuta hifadhi.

Aliongeza kuwa asilimia 80 ya hospitali hiyo haina huduma, na kwamba mamia ya watu waliuawa au kujeruhiwa katika mlipuko huo.
Alisema hospitali hiyo ilikuwa tupu huku watu wakiendelea na shughuli ya kuwaokoa manusura wa shambulio hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad