Cristiano Ronaldo Acheka Tuzo ya Messi


Cristiano Ronaldo achekeshwa na maneno ya muandishi wa habari aliyekuwa akiuzungumzia ushindi wa Ballon d'Or ya nane ya Messi na kuutafsiri kama "Upendeleo".

Ronaldo aliweka comment hiyo kwenye ukurasa wa @astelevision uliyemuonyesha mwanahabari Tomas Roncero, akisema kuwa;

Habari, Tulichodhani kuwa wanaenda kumpa Ballon d’Or nyingine Messi, kimetokea.

Alishinda Kombe la Dunia, ndio, lakini kwa penalti 6. Kombe la Dunia lilikuwa miezi 10 iliyopita, na sasa tuko Novemba. Messi ana Ballon d'Or nane, lakini anapaswa kuwa nazo tano, ana Ballon d'Or ya Andres Iniesta na Xavi, Robert Lewandowski ambaye alishinda mataji sita katika msimu mmoja na Haaland ambaye alikuwa mfungaji bora kwenye kila Ligi aliyoshiriki. "

Ronaldo ali-like chapisho hilo lenye utata, na kuacha comment ya emoji nne za kucheka. Comment hiyo ya mshambuliaji huyo wa Al-Nassr tayari ina Like zaidi ya 90,000 Instagram.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad