Muhtasari
• "Mpaka kufikia mwaka huu nilikuwa nimeshapanga kwamba sitakuwa tena nasafiria ndege za biashara," alisema.
• "Mpaka kufikia mwaka huu nilikuwa nimeshapanga kwamba sitakuwa tena nasafiria ndege za biashara," alisema.
Diamond
Msanii Diamond ambaye amekuwa akizunguka mataifa mbali mbali kwa kutumia ndege ya kibinafsi kwa mara ya kwanza amefufua uvumi kuhusu umiliki wa ndege yake ya kibinafsi ambao ulizagaa mwaka jana.
Diamond alikuwa anazungumza na waandishi wa habari baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kahama kwa ajili ya tamasha la Wasafi Festival ambapo aliulizwa kuhusu uwepo wa ndege yake ya kibinafsi kama alivyowaaminisha mashabiki wake mwaka jana.
Msanii huyo alifichua kwamba alipigwa usinga wa kichawi na kuingizwa mjini na watapeli ambao walimuahidi ndege na baada ya kuwapokeza hela Zaidi ya bilioni 4 za kitanzania, wakachimba mitini na kusangarai.
Hata hivyo, msanii huyo aliweka wazi kwamba mamlaka husika katika serikali ya Tanzania inajua hilo na inaendelea kufuatilia ili bilioni zake 4 zipate kurejea au apate ndege yake ya kibinafsi.
“Suala liko lakini [watapeli] wametuchelewesha sana. Sisi tulitakiwa tuwe na ndege yetu zamani sana tuwe tunazunguka nayo. Mpaka kufikia mwaka huu nilikuwa nimeshapanga kwamba sitakuwa tena nasafiria ndege za biashara, nilikuwa nataka nisafiri na ndege yangu tu,” alisema.
“Mimi nilikuwa nimenunua [ndege] kubwa ya kwangu ila wakaniletea ujanja wakaniingiza mjini kidogo wakanipiga kama bilioni 4 na kitu. Polisi wanafahamu na inaendelea kufuatiliwa na serikali wananisaidia kuona haki yangu naipata aje,” aliongeza.
Msanii huyo alisema kwamba ameshaanza kurudishiwa kidogo hela hizo na anaamini mwisho wa siku atapokea hela zake zote ili kuendelea na ndoto yake ya kumiliki ndege ambayo alisema kuwa haitakuwa yake pekee bali pia watu wengine watakuwa na uwezo wa kuikodisha na kuitumia vile vile.