Usiku wa kuamkia leo Jijini Kigali Rwanda zimetolewa Tuzo za Muziki za #TraceAwards2023 ambapo Tanzania imewakilishwa na Diamond Platnumz @diamondplatnumz, Zuchu @officialzuchu na Juma Jux @juma_jux , huku Mataifa mengine yakiwakilishwa na Mastaa kama Davido, Rema, Yemi, Burna, Fally n.k
Kutoka Tanzania Diamond ameipeperusha bendera ya Taifa vile inavyotakiwa Kwa kushinda tuzo kupitia kipengele cha Msanii Bora Afrika Mashariki.
Washindi wengine wa tuzo hizo ni Msanii Bora Ufaransa na Ubelgiji - Tayc (Ufaransa), Msanii Bora Uingereza - Central Cee, Msanii Bora Caribbean - Rutshelle Guillaume (Haiti), Msanii Bora Ukanda wa Bahari ya Hindi - Goulam (Comoro), Msanii Bora Brazil - Ludmilla, Msanii Bora Afrika Kaskazini - Dystinct (Morocco), Msanii Bora Nchi za Kifaransa - Didi B (Ivory Coast), Msanii Bora Rwanda- Bruce Melodie.
Wengine ni Msanii Bora wa Gospel - KS Bloom (Ivory Coast), Msanii Bora wa Live - Fally Ipupa (DRC), Dansa Bora - Robot Boli (Afrika Kusini), Msanii Alieleta Mabadiliko - Mr Eazi (Nigeria), Tuzo ya Heshima - 2Face, Msanii Bora wa Kike - Viviane Chidid (Senegal), Msanii Bora wa Kiume Ulimwenguni - Rema (Nigeria), Albamu Bora ya Mwaka - Love Damini (Burna Boy).
Msanii Bora Chipukizi- Roselvne Lavo (Ivory Coast), Wimbo Bora wa Kushirikiana - Unavailable (Davido x Musa Keys), Di Bora - Michael Brun (Haiti) Producer Bora - Tam Sir (Ivory Coast), Wimbo Bora wa Mwaka - Calm Down (Rema) na Video Bora ya Mwaka - Baddie - Yemi Alade (Nigeria).