Fei Toto Hatari Sana, Airejesha Azam FC kileleni Ligi Kuu


Fei Toto Hatari Sana, Airejesha Azam FC kileleni Ligi Kuu

Fei Toto Hatari Sana, Airejesha Azam FC kileleni Ligi Kuu


NYOTA wa Azam, Feisal Salum 'Fei Toto' ameirejesha timu hiyo kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuwawezesha matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Coastal Union.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, nyota huyo wa zamani wa Yanga alifunga bao hilo dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza hivyo kufikisha mabao manne ya Ligi Kuu Bara akiwa na timu hiyo.

Fei Toto kabla ya kufunga leo mchezo wa mwisho kwake ulikuwa dhidi ya Tabora United Agosti 16, wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-0 huku akionyesha kiwango kizuri baada ya kufunga matatu 'Hat-Trick'.

Kichapo hiki kinaifanya Coastal Union kupoteza mchezo wa tatu kati ya mitano iliyocheza huku miwili ikiisha kwa sare hivyo kuifanya kuendelea kutoonja ladha ya ushindi msimu huu chini ya Mkongomani, Mwinyi Zahera.

Kwa upande wa Azam huu ni ushindi wa nne kati ya michezo mitano iliyocheza na kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kufikisha pointi 13 na kuishusha Simba ambayo ilikuwa inashikilia usukani na pointi 12.

Azam imeendeleza ubabe mbele ya Coastal Union kwani mchezo wa mwisho uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Juni 6, mwaka huu iliondoka pia na pointi tatu baada ya ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Idris Mbombo na Prince Dube.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad